DAGE school TUNAFUNDISHA KOZI GANI?

Sinza,africa sana,Dar es salaam, Tanzania

Tufahamu vizuri DAGE

Tunafanya nini?

DAGE school of hair dressing and beauty ni chuo cha urembo kinachopatikana maeneo ya sinza africa sana mkabara na CRDB BANK tawi la mwenge,chuo chetu kinatoa mafunzo kwa kozi zifuatazo;
>> Kupamba kumbi za sherehe,mikutano n.k.
>> Urembo wa nywele,ngozi na kucha.
>> Mafunzo ya ujasiliamali na kujitambua (lifeskills).
>> Mafunzo ya kompyta.
>> Kuremba maharusi.

Sisi ni nani?

Neno DAGE ni kifupi cha maneno ya kiingereza ambayo ni "Development acquired general education",Ikiwa na maana kuwa "Maendeleo yanayopatikana kwa njia kuu ya elimu".Chuo hiki cha urembo DAGE kilianzishwa mnamo mwaka 2012 na kusajiliwa VETA kwa usajili namba VETA/DSM/2012/004.Chuo hiki kilianziswa na mwanamke anayefahamika kwa jina la Ms.Genoveva Kiliba ambaye aliitazama fulsa hii kwa kuanzia mbali sana na hata kufikia kuanzisha chuo hiki cha urembo, Lengo kuu la mwanamke huyu lilikuwa kuwasaidia wasichana wadogo wanaoishi katika mazingira magumu,wasiojua wafanye nini ili kutimiza ndoto zao.Chuo chetu kina waalimu na wakufunzi waliobobea katika fani mbalimbali za urembo,upambaji,ujasiliamali na stadi za maisha pamoja na walimu wa kompyuta.
karibuni sana

# Maudhui yetu

Chuo chetu cha urembo kilichopo sinza africa sana kina toa huduma za mafunzo kwa ngazi ya cheti katika urembo wa nywele,ngozi pamoja na kucha,upambaji kumbi,stadi za maisha afya n.k. Chuo kina pokea wanafunzi kuanzia waliomaliza darasa la saba mpaka chuo kikuu,Chuo kinazo hosteli nzuri sana kwa gharama nafuu kabisa
mnakaribishwa wote...

# Madhumuni yetu

Kama taasisi ya chuo cha DAGE tunayo madhumuni makubwa sana kwaaajili ya kukifanya chuo chetu kifahamike na kueleweka vizuri ndani na nnje ya mipaka ya nchi yetu,Hivi punde tunatazamia kufungua muhula wa masomo kwa ngazi ya stashahada (Diploma), na kwa kwadri MUNGU atakavyozidi tupatia uhai kama DAGE school of hair dressing and beauty tunatazamia pia kufungua usajili wa mafunzo ya urembo katika ngazi nyingine kubwa ya shahada (Degree).
karibuni sana.....

Picha zetu mbalimbali

Angalia video zetu ufahamu vizuri kuhusu Dage school of hair dressing and beauty

Dage school of hair dressing and beauty tunapatikana katika mitandao yote ya kijamii ikiwemo facebook,twitter,instagram,pamoja na youtube account ambapo tunaweka matangazo yetu mbalimbali,Tufuatilie kwa ukaribu ufahamu mengi kuhusu chuo chetu cha urembo Bonyeza hapa kupata mwongozo wa chuo chetu.

kwa habari ya youtube account yetu tufuatilie kwa kubonyeza kitufe hapo chini.

share,like na subscribe

Tutafute kwenye ramani na Tutumie ujumbe

M