Sisi ni nani?
Neno DAGE ni kifupi cha maneno ya kiingereza ambayo ni "Development acquired general education",Ikiwa na maana kuwa "Maendeleo yanayopatikana kwa njia kuu ya elimu".Chuo hiki cha urembo DAGE kilianzishwa mnamo mwaka 2012 na kusajiliwa VETA kwa usajili namba VETA/DSM/2012/004.Chuo hiki kilianziswa na mwanamke anayefahamika kwa jina la Ms.Genoveva Kiliba ambaye aliitazama fulsa hii kwa kuanzia mbali sana na hata kufikia kuanzisha chuo hiki cha urembo,
Lengo kuu la mwanamke huyu lilikuwa kuwasaidia wasichana wadogo wanaoishi katika mazingira magumu,wasiojua wafanye nini ili kutimiza ndoto zao.Chuo chetu kina waalimu na wakufunzi waliobobea katika fani mbalimbali za urembo,upambaji,ujasiliamali na stadi za maisha pamoja na walimu wa kompyuta.
karibuni sana